Jaza fomu hii kwa usahihi. Mwisho wa kujaza fomu ni tarehe 16/12/2025 - Saa 6 Usiku, kikao cha washiriki wote kitafanyika 13/12/2025 Kuanzia saa 2 asubuhi.
DAMUSSA ni Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule za Sekondari Mkoa wa Dar es Salaam. Kwa zaidi ya miaka 30 DAMUSSA imekuwa ikiandaa programu mbalimbali kwa ajili ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule za Sekondari za Dar es Salaam ili kuwapa miongozo mizuri ya Kimaadili na Kitaaluma.
DAMUSSA imeandaa semina na kambi kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza au Pre form one hadi kidato cha sita. Semina inatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku kumi (10) katika kipindi cha likizo ya mwezi wa kumi na mbili kuanzia 18-12-2025 hadi 27-12-2025 katika shule ya IHSAN ISLAMIC SECONDARY Kigamboni.